Skip to content

NuruProgramming/nyaraka

Repository files navigation

Nyaraka rasmi za Nuru

Hii ni hazina inayobeba nyaraka rasmi za Nuru.

Kupakua hazina hii

Hili upakue hazina hii, kwenye tamino ya tarakilishi(kompyuta) yako, fuata maelekezo yafuatayo.

  1. Kama unatumia SSH
git clone git@github.com:NuruProgramming/nyaraka.git
  1. Kama hutumii SSH
git clone https://github.com/NuruProgramming/nyaraka.git

Vile vile unaweza kupakua moja kwa moja kutoka GitHub kwa kutumia vitufe kama ilivyo kwenye picha hapa chini.

Pakua

Kufungua na kuanzisha

Kuweza kuifungua katika tarakilishi(kompyuta) yako, hakikisa umesanikisha Node.js v16+. Katika tamino yako tumia maelekezo yafuatayo ambayo yatasakinisha vitegemezi vya hazina hii;

npm i

Ikishamaliza kusanikisha, tumia maelekezo yafuatayo kuanzisha hazina hii iliuweze kuifungua kwenye kivinjari chako.

npm run docs:dev

Kuchangia

Ili kuchangia katika hizi nyaraka, tengeneza tengeneza tawi (fork) katika akaunti yako na fuata maelekezo ya kupakua hapo juu.

Ongeza mabadiliko yako, thibitisha (commit) na itume (push) kwenye GitHub.

git add -am "Tafsiri Nyaraka kwa kibena"
git push -u origin <TAWI LAKO>

Fungua Ombi la Kukubaliwa (Pull Request) kwenda kwenye nyaraka rasmi za Nuru

Unaweza pia kuchangia kwa kuongeza, kuboresha au kusahihisha matatizo katika sehemu ya matatizo (issues).

Releases

No releases published

Packages

No packages published